Skip to main content

MONUSCO yachukua hatua kuimarisha utoaji wa haki kwa watoto DRC

MONUSCO yachukua hatua kuimarisha utoaji wa haki kwa watoto DRC

Huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO kwa kushirikianana asasi isiyo ya kiraia AJEDEC na serikali wameanza ujenzi wa mahakama wilaya kwenye jimbo la Ituri.

Mahakama hiyo inalenga kuimarisha usimamiaji wa haki na sheria kwa kesi zinazohusu watoto hususan visa vinavyohusiana na ulinzi wa mtoto.

MONUSCO imegharimia mradi huo kwa dola zaidi ya elfu 37 ilhali mchango wa ndani ya nchi ni dola elfy mbili.

Uzinduzi wa ujenzi huo uliongozwa na mkuu wa ofisi ya MONUSCO huko Ituri Karna Soro na waziri wa mambo ya ndani wa DRC Unega Ege Etienne.