Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanasiasa msichana chipukizi alonga ‘’Wanawake msibweteke muhimu ni nidhamu’’

Mwanasiasa msichana chipukizi alonga ‘’Wanawake msibweteke muhimu ni nidhamu’’

Tunapomulika siku ya wanawake duniani leo Machi nane, ni muhimu tumulike wanawake waliopiga hatua katika nyanja tofauti. Kutana na Zainab Abdallah Issa, mwanasiasa chipukizi nchini Tanzania na aliye mkuu wa wilaya mdogo zaidi.

Aliteuliwa mwaka jana kuwa mkuu wa wilya ya Pangani akiwa na umri wa miaka 23, hatua iliyoshangaza wengi. Yeye anaiona kama fursa itokanayo na maono aliyonayo. Anamweleza Kelvin Mpinga wa redio washirika Pangani Fm ya Tanga Tanzania kwamba wanwake wengi wamebweteka wakitaka kutumia ngazi ya mafaniko ya wanaume kujinufaisha. Anaanza kueleza kulikoni akashika nafasi hiyo katika umri mdogo?