Kidole kimoja hakivunji chawa,wanawake waambiwa waungane

8 Machi 2017

Kuwa na virusi vya Ukimwi VVU, haikuwazuia kikundi cha wanawake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC kujiendeleza kiuchumi. Ndivyo unavyoweza kusema ukitafakari juhudi za wanawake katika ulimwengu wa kazi unaobadilika, ambapo licha ya hali zao hizo za kiafya, wanawake katika kikundi kiitwacho GSV jimboni Kivu ya Kusini, wamenufaika kwa mradi wa majiko.

Langi Stany Asumani anazungumza na kiongozi wa kikundi hicho anayedadavua namna umoja ulivyo nguzo katika mradi huo pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud