Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake shupavu waenziwa Uganda

Wanawake shupavu waenziwa Uganda

Uganda nayo imejiunga na Dunia kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake ambako wanawake zaidi ya hamsini wamepatiwa medali ya kuwaenzi kwa ushupavu wao katika nyanja mbalimbali. Shuhuda wetu hujo ni John Kibego.

(TAARIFA YA KIBEGO)

Nats!

Miongoni mwa waliopatiwa midali ni mwanajeshi mwanmke wa cheo cha juu zaidi katika historia ye jeshi la Uganda.  Huenda akawa pia ni wa kwanza bara Afrika kwani hakuna mwingine anayefahamika.

Maj. Gen. Proscovia Nalweyiso alitoa salamu kwa waliohudhuria.

(Sauti ya Maj. Gen. Proscovia)

“Napenda kuwasalimu nyoye na Kamanda Mkuu wetu, na nawapongeza nyota mliojitokeza kusherelekea Siku ya Wanawake Duniani. Nakutakieni madhimisho mema”

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni alisisitiza kuwa serikali inajitahidi kujenga miuondombunu ya kuwezesha zaidi wanawake.

(Sauti ya Museveni)

“Unapojadili masuala ya wanawake, isiyatenganishe na matatizo mengine katika jamii. Hauwezi kuwezesha wanawake bila kushughulikia masuala mengine. Wanawake watalindwa vipi wakati wa mzozo?”

Maadimisho ya taifa yalifanyika katika wilaya ya Ddokolo Kaskazini mwa nchi.