Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usawa wa kijinsia ni chachu katika kukomesha njaa na umasikini-UM

Usawa wa kijinsia ni chachu katika kukomesha njaa na umasikini-UM

Shirika la chakula na kilimo FAO kwa ushirikino na mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD na shirika la mpango wa chakula duniani WFP, wamechagiza juhudi katika kuhakikisha usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake hasa wa vijijini, masuala ambayo wanasema ni chachu ya kukomesha njaa , utapia mlo na umasikini.

Kauli hiyo imetolewa kwenye hafla maalumu ya maadhimisho ya siku ya kiamtaifa ya wanawake iliyofanyika katika makao makuu ya mashirika hayo mjini Roma Italia.

Akisistiza umuhimu wa kundi hilo la wanawake mkurugenzi mkuu wa FAO Jose Graziano da Silva amesema

(SAUTI YA GRAZIANO)

“Mwanamke ana jukumu kubwa katika kilimo na mfumo wa chakula, sio tu kama wakulima bali pia kama watayarishaji, wafanyabiashara na wazimamizi, hata hivyo wanawake bado wanakabiliwa na vikwazo vingi katika soko la ajira vijijini na katika fursa za kilimo. Wanawake wanauwezekano mkubwa wa kufanya kazi zenye ujira mdogo bila kuwa na ulinzi wowte wa kijamii au kisheria.”

Akaenda mbali zaidi na kuongeza

(SAUTI YA GRAZIANO)

“Hii inabana uwezo wa mwanamke kujiendelea kiujuzi, kipato na fursa za ajira. Ninashawishika kwamba mustakhbali wa uhakika wa chakula kimataifa unategemea uwezeshaji wa uwezo wao, hili linatambuliwa na ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu, kufikia usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake ni kiungo muhimu katika vita dhidi ya umasikini, njaa na utapia mlo.”