Skip to main content

Jamii zetu zitakuwa thabiti iwapo tutashirikisha wanawake- Guterres

Jamii zetu zitakuwa thabiti iwapo tutashirikisha wanawake- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema ulinzi wa wanawake dhidi ya ukiukwaji wa haki zao pamoja na umaskini vitawezekana iwapo watapatiwa kipaumbele kamilifu kwenye mipango ya kuwawezesha.

Akizungumza mjini Nairobi, Kenya ambako yuko ziarani, Bwana Guterres amesema ujumuishaji huo uhakikishe wamo kwenye taasisi za serikali, siasa na biashara bila kusahau bodi za kampuni na michakato ya amani.

Amesema Umoja wa Mataifa unaamini kuwa uwepo wa wanawake katika maeneo hayo utawezesha maendeleo kuwa thabiti na endelevu, amani itakuwa rahisi kulindwa na haki za binadamu zitalindwa.

Katibu Mkuu amepongeza Kenya kwa jinsi ilivyoweka mipango ya kuwezesha wanawake kwa maslahi ya taifa hilo na bara zima kwa ujumla.