Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika ionekane kama bara la mafanikio sio matatizo tu-Guterres

Afrika ionekane kama bara la mafanikio sio matatizo tu-Guterres

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres anayeendelea na ziara yake nchini Kenya amesema anaamini kwamba simulizi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika haijakuwa sawa wakati wote, kwani wakati mwingine imejikita sana katika mogogoro .

Akiongeza kuwa ni kweli kwamba kuna migogoro Afrika kama ilivyo barani Ulaya au Asia, kuna migogoro kila kona, akasisitiza lakini Afrika ni lazima ionekana zaidi na zaidi kama bara la mafanikio na fursa.

Guterres ameyasema hayo kwenye mkyutano na waandishi wa habari baada ya mazungumzo yake na Rais Uhuru Kenyatta ikulu ya Nairobi , ambapo amelishukuru taifa hilo kwa mchango wake kwenye vikosi vya ulinzi wa amani, AMISOM na kwenye Umoja wa Mataifa, mchango wake katika suala zima la wakimbizi na kwa ushirikiano baiana ya Kenya na Umoja wa Mataifa. Amesema taifa hilo ni mfano wa kuigwa kwa sababu..

(SAUTI GUTERRES)

“Hakuna nchi kama Kenya, ni ishara ya mafanikio na fursa hizo za Afrika, sio kwa sababu ya uwezo wake wa utawala, lakini kwa sababu ya jumuiya zake za kiraia, jumuiya zake za kibiashara na uhuru wa vyombo vya habari. Kenya ni mfano kwa nyanja zote ambao unaweza kuigwa sio tu barani Arika lakini duniani kote ikizingatiwa kwamba katika dunia ya leo kuna nchi zinajitahidi kuhakikisha kwamba nguzo tatu za shughuli za Umoja wa mataifa zinafikiwa , ambazo ni amani na usalama, maendeleo endelevu yaliyo jumuishi na haki za binadamu.”

Naye Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akizungumzia suala vita dhidi ya ugaidi wa al- Shabaabu na wakimbizi wa Somalia kwenye kambi ya Dadaab amesema Katibu mkuu

(CUT UHURU KENYATTA)

“Alikuwa mwepesi kutuhakikishia na kuihakikishia jumuiya ya kimataifa , kwamba atafanya kazi nasi kuwasaidia wakimbizi wa Somalia na nilitiwa moyo pia na msaada uliotolewa na Katibu Mkuu kuhusu mpango wa ulinzi wa amani wa Muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM, tunaamini kwamba endapo utaimarishwa ipasavyo , basi tutamaliza moja kwa moja tishio linalowekwa na wanamgambo wa Al- Shabaabu Somalia na kwenye ukanda wetu.”