Kila mtoto anastahili kuishi kwa usalama: UNICEF

7 Machi 2017

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Anthony Lake amesema kuwa watoto wakimbizi wanaokimbia machafuko na ugaidi hivi sasa wanahitaji

msaada kuliko wakati mwingine wowote. Lake ametoa kauli hiyo kufuatia  amri mpya nyingine ya Marekani iliyotolewa  Jumatatu kuhusu wanaosaka hifadhi na ukimbizi.

Amesema watoto ni miongoni mwa watu wanaoishi katika mazingira magumu na waathirika wakubwa duniani. Ameongeza kuwa UNICEF itaendelea kushirikiana na Marekani na washirika wengine ili kuwasaidia.  Ameelezea matumaini yake kuwa hatua hii itakuwa ya muda mfupi na kwamba Marekani itaendelea na utamaduni wake wa muda mrefu wa kuwalinda watoto wanaokimbia vita na mateso kwani kila mtoto anastahili kuishi katika hali ya  usalama.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter