Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na AU wazindua ripoti ya haki za wanawake Afrika

UM na AU wazindua ripoti ya haki za wanawake Afrika

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa , Muungano wa Afrika na kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya wanawake UN Women, leo wamezindua ripoti kuhusu haki za wanawake Afrika.

Hii ni ripoti ya kwanza katika mfululizo uliopangwa kuhusu haki za wanawake katika bara hilo itaklayojikita katika mada mbalimbali. Mashirika hayo yamesema kuna hatua kubwa zimepigwa katika kutambua haki za wanawake barani afrika, kwa mfano ushiriki wa wanawake katika bunge Afrika unapita ule wan chi nyingi zilizoendelea.

Wameongeza kuwa hata sheria zimebadilika kwani sasa kuna sheria nyingi katika katika kuhusu masuala ya ukatili wa kingono na wa majumbani, haki za uchumi,kijamii na kitamaduni na za kupinga ubaguzi.

Hata hivyo wamesema katika kila nchi barani Afrika kama ilivyo kote duniani wanawake wanaendelea kunyimwa fursa ya kufurahia haki zao. Twakwimu katika ripoti hiyo zinasema katika nchi sita hakuna ulinzi wa kisheria kwa wanawake dhidi ya ukatili majumbani . Mwaka 2013 wanawake na wasicha Afrika walikuwa ni asilimia 62 ya watu wote waliokufa kutokana na matatizo yanayozuilika ya ujauzito na kujifungua, huku takribani wanawake na wasichana milioni 130 wamepitia ukeketaji, hasa barani Afrika.

Ripoti hiyo imeonya kwamba endapo mwenendo wa sasa utaendelea , basi karibu nusu ya maharusi watoto ifikapo mwaka 2050 watakuwa Waafrika.