Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

SDGs bila takwimu haiwezekani: Montiel

SDGs bila takwimu haiwezekani: Montiel

Ikiongozwa na kauli mbiu, takwimu bora maisha bora, tume ya takwimu ya Umoja wa Mataifa imeanza kikao chake cha 48 hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika idara ya uchumi na masuala ya kijamii Lenni Montiel, amesema takwimu ni muhimu katika katika kutimiza ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu katika maeneo kadhaa.

Ameitaka tume hiyo itakayiokutana kwa siku nne kutumia fursa hiyo kuchochea utekelezaji wa ajenda hiyo akisema.

( Sauti Montiel)

‘‘Ajenda ya 2013 0 inathitajai takwimu katika maeneo mengi ili kutumika kwa makundi tofauti kama jinsia, umri, ukabila, hadi za uhamiaji, ulemavu , kipato, maeneo  ya kijografia na maengineyo ili kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma.’’ 

Hakusita kuzungumzia faraja yake ya uwakilishi mkubwa wa wanawake katika mkutano huo sambamba na maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mnamo Machi nane.

( Sauti Montiel)

‘‘Napenda kutizama mabadiliko mujarabu ya uwakilishi wa wanawake katika tume ya takwimu ikilinganishwa na tume ilipoanza mwaka 1947. Kumekuwa na mabadiklio makubwa sio tu katika uwakilishi wa wanawake lakini pia njia zitumikazo katika jukumu la wanawake katika takwimu kitaifa.’’