Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres alaani kitendo cha DPRK kurusha makombora

Guterres alaani kitendo cha DPRK kurusha makombora

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres amelaani kitendo kilichoripotiwa cha Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK kurusha makombora manne ya masafa marefu.

Imeelezwa kuwa makombora matatu kati ya hayo manne yametua baharini kwenye ukanda mahsusi wa kiuchumi wa Japan.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemnukuu Katibu Mkuu akisema vitendo vya namna hiyo ni ukiukaji wa maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na vinadhoofisha amani na usalama wa kikanda.

Katibu Mkuu amerudia wito wake kwa uongozi DPRK uongozi kujiepusha na vitendo zaidi vya uchochezi na kuzingata wajibu wake wa kimataifa.