Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MINUSMA yalaani ukiukwaji wa kusitisha mapigano Timbuktu Mali

MINUSMA yalaani ukiukwaji wa kusitisha mapigano Timbuktu Mali

Vituo viwili vya kijeshi vilivyokuwa vinashika doria vimeshambulia  jana jumapili na kikundi cha waasi wenye silaha huko kaskazini mwa mji wa Timbuktu nchini Mali.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSMA ambao unasema kuwa vikundi hivi vyenye silaha vinapinga uanzishwaji wa serikali ya mpito ya Taoudenit, iliyokuwa imepangwa kuanza leo. Uanzishwaji wa mamlaka hiyo  ni hatua muhimu katika utekelezaji wa mkataba wa amani na maridhiano nchini Mali.

MINUSMA imealaani vikali vitendo hivyo ikitaja kuwa ni ukiukaji wa usitishaji mapigano na wahusika wanaweza kuwekewa vikwazo.

Tayari ujumbe huo umeanzisha mazungumzo mara moja kupunguza mvutano na umetoa wito kuondolewa kwa haraka na bila masharti msimamo wa vikundi hivyo. MINUSMA pia imechukua hatua ili kuhakikisha ulinzi wa raia.