Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasomali wanahaha kukidhi mahitaji ya mlo kwa familia- O'Brien

Wasomali wanahaha kukidhi mahitaji ya mlo kwa familia- O'Brien

Mratibu Mkuu wa masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa Stephen O’Brien ametembelea makazi ya muda ya wakimbizi wa ndani yaliyoko nje kidogo ya mji mkuu wa Somalia, Mogadishu ambako amejionea hali halisi ya njaa inayokabili nchi hiyo.

Ameshuhudia jinsi familia zinavyohaha kukidhi mahitaji ya mlo ya watoto wao akisema kwa kujionea mwenyewe, amepata uwezo zaidi wa kupaza sauti ili misaada iweze kufikia wahitaji hao haraka iwezekanavyo.

Kwa sasa wasomali milioni 6.2 wanahitaji misaada ya kibinadamu ambapo kati yao hao milioni tatu wanahitaji msaada wa haraka wa kuokoa maisha yao, hivyo Bwana O’Brien anasema..

“Popote pale unapokuwa na mazingira ambamo kwayo watu wanahaha kukidhi mahitaji yao waishi au kulindwa dhidi ya mzozo, lazima utapata wakimbizi wa ndani, na hapa tuna mwelekeo mkubwa wa ukimbizi wa ndani. Kuna umuhimu wa kuchukua hatua sasa na kwa pamoja ili kufadhili mipango inayoweza kusaidia zaidi wakati huu wa uhitaji.”