Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haiti inahitaji msaada wa ujenzi mpya-UNISDR

Haiti inahitaji msaada wa ujenzi mpya-UNISDR

Wito wa msaada wa ujenzi mpya kwa ajili ya Haiti umetolewa jumatatu na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na udhibiti wa athari za majanga UNISDR baada ya kimbunga Matthew kuliacha taifa hilo na hasara ya dola bilioni 2.7. Rosemary Musumba na taarifa kamili.

(TAARIFA YA ROSE)

Msaada huo wa haraka ni kwa ajili ya kuboresha mifumo ya udhibiti wa majanga baada ya ripoti ya kimbunga Matthew cha miezi sita ilityopita kubainisha ukweli kwamba Haiti haina uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na majanga yatokanayo na hali ya hewa.

Kwa mujibu wa mkuu wa UNISDR Robert Glasser wakati mifumo ya serikali ilisaidia kupunguza idadi kubwa ya vifo , lakini ni suala lisilokubalika kwa watu zaidi ya 600 kupoteza misha kwenye kimbunga hicho.

Bwana Glasser ametoa wito wa msaada wa mipango ya ujenzi mpya iliyoandaliwa na serikali ya Haiti, Umoja wa mataifa na wadau wengine ambayo inahitaji dola bilioni 2.72 kwa miaka mitatu ijayo.