Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunza sikio kama yai kwani likishaharibika ndio basi- WHO

Tunza sikio kama yai kwani likishaharibika ndio basi- WHO

Zaidi ya asilimia tato ya watu wote duniani wanaishi na tatizo la kupoteza uwezo wa masikio kusikia, lakini kuzuia tatizo hilo ni rahisi kuliko kuitibu.

Hayo ni kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO katika ujumbe wake kuhusu siku siku ya kimataifa ya uwezo wa masikio kuiskia duniani . Kauli mbiu mwaka huu ikiwa ni kuchukua hatua na kuwekeza katika kutatua tatizo la uwezo wa sikio kusikia.

Dr Shelly Chadha, mtaalamu wa upotevu wa uwezo wa sikio kusikia kutoka Who anasema zaidi ya vijana na barubaru bilioni moja wako katika hatari ya kupoteza uwezo wa sikio kusikia kutokana na kusikiliza muziki kwa sauti ya juu lakini

(SAUTI DR CHADHA)

“Kuzuia inawezekana na inafanikiwa lakini kuponya au kutibu haiwezekani kwa mantiki kwamba huwezi kugeuza upotevu wa uwezo wa sikio kuiskia uliosababishwa na kusikiliza sauti ya juu”