Skip to main content

Mabadiliko ya tabia nchi huathiri watoto zaidi:UM

Mabadiliko ya tabia nchi huathiri watoto zaidi:UM

Mabadiliko ya tabia nchi yanatoa tishio kubwa kwa watoto, limeelezwa baraza la haki za binadamu Alhamisi.

Katika mjadala uliofanyika Geneva, nchi wanachama na wataalamu wa haki za binadamu wameonya kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanatishia mafanikio ya vijana katika fursa ya chakula, maji , afya na elimu.

Na suluhu kwa mujibu wa wataalamu hao ni kuhusisha miradi ya kiwango kidogo cha uchaguzi wa hewa ili kuchagiza maendeleo endelevu. Makadirio ya shirika la afya ulimwenguni WHO yansema matatizo ya chakula yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi yataweza kukatili maisha ya watoto na vijana 95,000 ifikapo mwaka 2030.

Wajumbe wametanabaisha jinsi gani makundi yasiyojiweza yakiwemo ya masikini, wenye ulemavu, watoto wa jamii za watu wa asili na wasichana walivyo katika hatari kubwa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Naibu mwakilishi wa kudumu wa Ufilipino, Maria Teresa Almojuela, amesema suala hilo ni muhimu sana kwa nchi yake kwani imekuwa miongoni mwa walio katika hatari.

Mwaka 1995 hadi 2015 Ufilipino imekabiliwa na majanga ya asili zaidi ya 270 ambayo yamewaathiri watu zaidi ya milioni 250 kote duniani kwa mwaka.

Kwa upande wake Peggy Hicks, kutoka ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa ameliambia baraza la haki za binadamu kwamba mktaba wa Paris wa mabadiliko ya tabia nchi na malengo ya maendeleo endelevu SDG’s yamezitaka serikali kuchukua hatua kuhusu suala hili.