Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mavuno ni mengi lakini baa la njaa lashika kasi- FAO

Mavuno ni mengi lakini baa la njaa lashika kasi- FAO

Hali ya usambazaji chakula kote duniani imeimarika lakini upatikanaji wa chakula umepungua kwa kiasi kikubwa katika maeneo yanayokabiliwa na mgogoro huku ukame ukizidi kudororesha uhakika wa chakula katika nchi za Afrika Mashiriki.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la chakula na kilimo duniani FAO kwenye ripoti yake mpya kuhusu matarajio na mwelekeo wa hali ya chakula.

Mkuu wa idara ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, FAO Kostas Stamoulis amesema baadhi ya nchi 37 zinahitaji msaada kutoka nje kwa ajili ya chakula, ambapo 28 kati ya hizo ziko Afrika, chanzo ni El nino ambayo iliathiri mavuno mwaka jana.

Amesema ingawa mavuno yanatarajiwa kuwa bora mwaka huu, bado kuzuka kwa viwavijeshi, pamoja na mafuriko nchini Msumbiji, Zambia na Zimbabwe vinaweza kuleta kikomo cha faida kubwa ya uzalishaji.