Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatutafikia SGD's iwapo hatutayawasilisha kwa kila mtu

Hatutafikia SGD's iwapo hatutayawasilisha kwa kila mtu

Tamasha la Kimataifa kuhusu Fikra linaendelea jijini Bonn, Ujerumani ambapo mada kuu iliyojadiliwa leo ni umuhimu wa utoaji wa habari na uwasilishaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDG's. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye idara ya habari na mawasiliano , Cristina Gallach amenieleza kuwa ili kusongesha mbele na kufikia malengo hayo, kitengo chake kilizangatia matumizi ya lugha na nembo zinazowasilisha SDG's, ili kuhakikisha malengo hayo 17 yanaujumbe uliorahisi kueleweka na katika lugha inayovutia, akiongeza kuwa sasa ni wajibu wa kila mtu kuwasilisha malengo hayo...

(Sauti ya Gallach 1)

" Kadri tunavyozidi kuwasilisha malengo ya maendeleo endeluvu na kufahamisha watu kuhusu ajenda hii, ndipo serikali zitawajibika zaidi na kuhakikisha yanatekelezwa".

Amefafanua mikakati walioyoweka kuhakikisha zinamfikia kila mtu..

(Sauti ya Gallac 2)

"Muhimu zaidi ni kuenda katika ngazi za mitaa, watu wahisi kuwa mambo yanafanyika, ili serikali za mitaa zitekeleze na vyombo vya habari nchini zifuatilie kile kinachoendelea"