Skip to main content

Wanawake wapatiwe tiba sahihi dhidi ya madawa ya kulevya- Ripoti

Wanawake wapatiwe tiba sahihi dhidi ya madawa ya kulevya- Ripoti

Ripoti ya mwaka 2016 ya Bodi ya kimataifa ya kuzuia madawa ya kulevya, INCB, imezinduliwa hii leo ambapo pamoja na mambo mengine imetaka serikali duniani zihakikishe kuwa sera zinazolenga udhibiti wa matumizi ya mihadarati zinajumuisha wanawake wakati huu ambapo idadi ya wanawake wanaotumia madawa hayo imeongezeka. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Ripoti hiyo ina sura nne ambapo sura ya kwanza iliyoangazia wanawake na mihadarani inasema kuwa theluthi moja ya watumiaji wa madawa hayo hivi sasa ni wanawake na wasichana huku wanaopatiwa matibabu ni moja ya tano kwa kuwa mifumo iliyopo inawaengua kupata tiba.

Wanawake wanahusika na usafirishaji wa madawa hayo na wanapokamatwa na kufungwa gerezani, wanakuwa katika nafasi kubwa zaidi ya kuanza kutumia madawa hayo kupita kiasi bila kusahau biashara ya ngono.

Mkurugenzi wa bodi hiyo Werner Sipp anasema hatma yake ni utegemezi huku mazingira ya matibabu yakiwa na vikwazo.

(Sauti ya Sipp)

“Tunatoa wito kwa wale wanaoweza kubadilisha hali hii kuchukua hatua kama vile kuboresha upatikanaji huduma za kinga au kuboresha huduma kwa kuweka vituo vingi zaidi mahsusi kwa ajili ya wanawake.”