Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Afrika ya mlo shuleni yaadhimishwa Brazzaville: WFP

Siku ya Afrika ya mlo shuleni yaadhimishwa Brazzaville: WFP

Siku ya Afrika ya mlo shuleni imezinduliwa rasmi na kuadhimishwa Machi mosi 2017 chini ya ulezi wa serikali ya Jamhuri ya Congo Brazzavile , ikiwa na kauli mbiu “Ulishaji mashuleni, ni uwekezaji kwa vijana kwa ajili ya kuimarisha mustakhbali wao” Rosemary Musumba na taarifa kamili

(TAARIFA YA ROSE)

Kwa mujibu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP ambalo limeshiriki kwa kiasi kikubwa kufanikisha mradio huo, siku hiyo ya kihistoria imesherehekewa pia na tume ya Muungano wa Afrika, nchi wanachama wa muungano wa Afrika na wadau wengine wa maendeleo ya elimu.

Maafisa wa serikali ya Congo Brazzaville , na mawaziri wa serikali mbalimbali zikiwemo Ethiopia, Guinea Bissau, Chad, Zimbabwe, Senegal, na wahisani wa maendeleo walikuwa miongoni mwa wageni.

Siku hiyo ilipitishwa rasmi na wakuu wan chi wanachama wa Muungano wa Afrika katika kikao chao cha 26 mwezi Januari 2016 kwa kutambua mchango mkubwa wa nchi husika kutoa mlo mashuleni kwa kuboresha kiwango cha elimu na kuongeza pato kwa jamii , na huu ni mwaka wa pili inaadhimishwa.