Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame ni janga la kitaifa Somalia: Rais Farmaajo

Ukame ni janga la kitaifa Somalia: Rais Farmaajo

Rais mpya wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmaajo ambaye aliapishwa hivi karibuni ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia taifa lake kukabiliana na ukame ulioathiri zaidi ya raia milioni sita.

Akizungumza mjini Mogadishu kwenye mkutano wa ngazi ya juu kwa ajili ya ukame ambao amesema ni janga la kitaifa, Rais Farmaajo ameomba jumuiya hiyo kuongeza mchango wao wa dola million 825 ili kuzuia janga linaloweza kutokana na baa la njaa.

(Sauti ya Farmaajo)

“Sisi tuliokusanyika hapa leo hatuwezi kuileta mvua wala maji ya kutosha ili mifugo iwe hai. Lakini tunawajibu kwa ufanisi zaidi kusaidia taifa la Somalia ambalo l ina tishio la njaa. "

Akizungumza kwenye mkutano huo naibu mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia ambaye pia ni mratibu wa misaada ya dharura  Peter de Clercq amesema ii kufanikisha hatua hiyo kinachotakiwa ni.

 (Sauti ya De Clerq)

“Utekelezaji wa msamaha wa kodi juu ya uagizaji wa vifaa muhimu ya kibinadamu ambayo bado inavutia aina yoyote ya kodi, kuiondoa kwa muda ya kodi na ushuru kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuwawezesha kuongeza utoaji wa misaada ya kibinadamu na kuimarisha usalama katika maeneo muhimu ya utoaji misaada ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa vizuizi haramu barabarani haramu, na hatua thabiti ili kuzuia kupelekwa kwingineko kwa misaada ya kibinadamu”.

Bwana de Clercq ametoa wito wahisani kuharakisha utoaji wa zaidi ya dola milioni 400 zilizoahidiwa ili kuruhusu washirika kuweza kuongeza kazi zao.

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema kwamba idadi ya wasomali wanaohitaji msaada imeongezeka kwa kasi katika miezi ya hivi karibuni kutoka milioni 5 Septemba mwaka jana hadi zaidi ya milioni 6.2.