Hali ya Yemen bado ni tete:O’Brien

Hali ya Yemen bado ni tete:O’Brien

Hali ya kibinadamu nchini Yemen bado ni tete na mamilioni ya watu wanahitaji msaada wa haraka hasa katika maeneo ya Kaskazini ambako hali ya usalama ni mbaya zaidi.

Akizungumza kwa jia ya video kutoka mjini Saana, Mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Stephen O’Brien amesema alipata fursa ya kuzuru Aden na maeneo mengine kujionea hali halisi.

Ameongeza kuwa bado misada ya kibinadamu haiajawafikia walengwa wote kutokana na hali ya usalama na vituo vya upekuzi hasa mjini Taiz inayofanya misafara ya misaada kushindwa kufika huko na ametoa wito kwa pande husika katika mzozo

(SAUTI YA O’BRIEN)

“Tumeweka bayana mtazamo wetu kwa waziri mkuu wa mamlaka ya Houthi hapa Sanaa na tumeahakikishiwa kwamba watafungua njia hususani kwa malori yaliyo na msaada wa WHO, hivyo tutasubiri kuona kama ahadi hiyo itatekelezwa katika siku moja ijayo au zaidi”

Pia amezungumzia suala la uwajibikaji kuhusu fedha za msaada dola bilioni mbili zilizotolewa

(O’BRIEN CUT 2)

Walimu elfu 21 tu ndio waliolipwa kwa mwezi mmoja hiyo ni sehemu ndogo tu ya dola bilioni mbili hivyo unauliza uwajibikaji na uwazi wa wapi fedha zingine zimekwenda hilo bado halijafanyika , kwa hakika kuna hali ngumu kwa wafanyakazi wa umma , na hili linaongeza madhila kwa watu hapa ambao wamejikuta katikati ya mgogoro wasiouanzisha.”