Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulizi dhidi ya Allepo ni uhalifu wa kivita: Ripoti

Mashambulizi dhidi ya Allepo ni uhalifu wa kivita: Ripoti

Mapigano ya kuudhibiti mji wa Aleppo nchini Syria mwaka jana, yamesababisha mateso makali yanayochochea uhalifu wa kivita wameonya leo wachunguzi wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.

Ikitumia shuhuda 300 za picha za setilaiti na sauti nyingine, ripoti ya kamisheni ya uchunguzi imeonyesha jinsi gani ndege za kivita za Syria na Urusi zilivyogeuza Mashariki mwa Aleppo kuwa mahame huku vikosi vya upinzani vikidaiwa kuporomosha mabomu katika maeneo yenye idadi kubwa ya watu ambayo yanadhibitiwa na vikosi vya serikali.

Ripoti hiyo ya13 ya kamisheni hiyo inaangazia uvinjifu wa haki za binadamu kufuatia machafuko mjini Allepo Syria, kati ya kipindi cha Julai hadi Disemba mwaka jana ambapo pia ulengaji wa maeneo ya huduma muhimu katika maeneo ya Mashariki mwa mji huo, yanayiodhibitiwa na waasi unamulikwa.

Mkuu wa jopo la uchunguzi Paulo Pinhiero amesema sio tu kuwa raia walishambuliwa vikali kupindukia, bali pia walikuwa walengwa.

( Sauti Pinhiero)

‘‘Ndege za kivita za Syria na Urusi bila kuchoka zilishambulia Mashariki mwa Aleppo ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kulazimisha kujisalimisha. Hospitali, vituo vya yatima, shule, masoko na nyumba ziliharibiwa.’’

Ameongeza kuwa baada ya vikosi vya serikali kuzingira Mashariki mwa mji huo mwezi Julai, mamia ya raia walifariki kwa kuvurumishiwa makombora mazito, yakiwemo ya kurushwa kutoka angani, silaha za kuunguza, silaha nzito na kemikali.