Machungu kabla ya kunyongwa ni makubwa- Zeid

1 Machi 2017

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad al Hussein amesema madhila wanayokumbana nayo wafungwa wanaosubiri adhabu ya kifo ni miongoni mwa sababu tosha za kuweza kuondokana na adhabu hiyo.

Akizungumza mjini Geneva, Uswisi wakati wa kikao cha ngazi ya juu kuhusu hoja ya adhabu ya kifo ambapo sasa Umoja wa Mataifa inapigia chepuo ipigwe marufuku, Kamishna Zeid amesema taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa kwa miongo kadhaa zimebaini kuwa..

(Sauti ya Zeid-1)

Ukatili wa adhabu ya kifo haupo tu kwenye kifo chenyewe na machungu yatokanayo nayo, bali pia athari zisizo za kiutu apatazo mtu wakati anasubiri kwa muda mrefu kabla ya kunyongwa.”

Hivyo amesema..

(Sauti ya Zeid-2)

“Machungu makubwa ya kifikra na kimwili yampatayo mhusika na familia yake kutokana na adhabu ya kifo sasa yanapaswa kujumuishwa kwenye uzito wa hoja.”

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter