Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu chanjo zinapotoshwa- WHO

Taarifa kuhusu chanjo zinapotoshwa- WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema linatiwa wasiwasi na upotoshwaji  wa habari kuhusu kinga kupitia tovuti kadhaa hatua ambayo shirika hilo imeliita hatari na kutaka wadau kupata taarifa sahihi. John Kibego na taarifa kamili.

(TAARIFA YA KIBEGO)

Katika kuhakikisha taarifa sahihi, WHO imeanzisha wavuti wa kimataifa kuhusu usalama wa chanjo uitwao VSN, ambao hadi sasa mtandao huo una wanachama 47  na unatumia lugha 12,  huku ikikadiriwa kuwa watu zaidi ya milioni 173  hutembelea wavuti huo kupata taarisa sahihi.

Mratibu wa wavuti huo Isabelle Sahinovica amesema wazazi, watoa huduma ya afya na wataalamu wengine wanahitaji kupata taarifa sahihi na za kuaminika kuhusu chanjo.

WHO hata hivyo imesisitiza kuwa uwepo wa wavuti husaidia kufanya uamuzi sahihi lakini ikaonya kuwa hiyo haimaanishi kwamba ni mbadala wa mazungmzo na  daktari kupata ufafanuzi.