Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tamasha la Fikra lafungua pazia leo huko Bonn

Tamasha la Fikra lafungua pazia leo huko Bonn

Tamasha la siku tatu lenye  lengo la kuchagiza mawazo mapya katika kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDG's lmeanza leo jijini Bonn, Ujerumani ambako mwandishi wetu Amina Hassan amepiga kambi na ametuletea ripoti hii.

(Taarifa ya Amina)

Akifungua tamasha hilo lijulikanalo kama "Tamasha la Kimataifa la Fikra" ambalo limeleta pamoja watunga sera, asasi za kiraia, vijana na mashirika kutoka mashinani, Mkurungezi wa Kampeni ya Umoja wa Mataifa kuhusu SDG's Mitchell Toomey akaanza kwa kusema "hatimaye tupo hapa"..

image
Sara Poole, (katikati) Naibu Msaidizi mkuu wa UNDP akicheza moja ya michezo ya kidijitali inayolenga kubonga bongo na kufanikisha SDGs. (Picha:Idhaa ya Kiswahili/Amina Hassan)
Naye Naibu Msaidizi Msimamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo, UNDP , Sara Poole akaeleza haja ya ufumbuzi wa ubunifu huo katika kuendeleza malengo ya maendeleo endelevu ..

(Sauti ya Sara)

 "Ili kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2030 SDGs itafikiwa, kwa kila mtu, kila mahali, ni lazima tuwe wabunifu kwa kila njia katika uwasilishaji wa malengo,kujenga ushirikiano, na kushinikiza watu zaidi kuchukua hatua katika ngazi za mitaa, kikanda na kimataifa. "

Na miongoni mwa walioshiriki ni Faustine P. Nyanda kutoka Tanzania na anasema kile anachokitarajia...

(Sauti ya Faustine).