Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utapiamlo huigharimu Pakistan dola bilioni 7.6 kila mwaka: WFP

Utapiamlo huigharimu Pakistan dola bilioni 7.6 kila mwaka: WFP

Madhara ya utapiamlo  ikiwa ni pamoja na gharama za juu za matibabu huigharimu Pakistan dola bilioni 7.6 sawa na asilimia tatu ya pato la taifa kila mwaka, imesema ripoti ya shirikal a mpango wa chakula duniani WFP.

Ripoti hiyo ilipewa jina Madhara  ya uchumi wa lishe Pakistan: Tathmini ya Hasara"imezinduliwa na na WFP kwa kushirikiana na tume inayoshughulika na masuala ya utapiamlo nchini humo na wizara ya mpango wa maendeleo na mageuzi.

Kwa mujibu wa ripoti, inakadiriwa kuwa zaidi ya watoto 177,000 hufa kila mwaka nchini Pakistan, kabla ya kufikisha miaka mitano kwa sababu wao au mama zao wana utapiamlo ambayo ni thamani ya karibu dola bilioni 2.24 ya nguvu kazi inayopotea kila mwaka. Kadhalika taifa hilo lina zaidi ya visa 90 milioni vya ugonjwa wa kuhara na madhara ya kupumua miongoni mwa watoto kutokana na ukosefu wa kunyonya maziwa ya mama ambapo dola bilioni 1 hutumika katiak mfumo wa afya kutibu magonjwa hayo.

WFP imesema kwamba zaidi ya theluthi mbili ya watoto wanasumbuliwa na kudumaa, upungufu wa damu au upungufu wa madini mwilini inayowaathiri katika maendeleo ya kiakili na kimwili hivyo kusababisha matokeo mabaya shuleni na na tija ya chini kama watu wazima inayopunguza pato dola bilioni 3.7 kila mwaka.