UM kutathimini haki za wazee Namibia

28 Februari 2017

Mtaalamu wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa Rosa Kornfeld-Matte anatarajia kufanya ziara ya kwanza ya kikazi nchini Namibia kuanzia Machi pili hadi 13 mwaka huu kwa ajili ya kutathimini hali ya haki za binadamu kwa wazee nchini humo.

Katika taarifa yake ya kulekea katika ziara hiyo, mtaalamu huyo amesema ni fursa muhimu ya kuanisha utekelezaji na upungufu wa sheria zilizopo zinazohusiana na kukuza na kulinda haki za wazee. ‘‘Nina shauku ya kujifunza kuhusu mfumo wa kina wa ulinzi wa kijamii wa Namibia, ikiwamo pensheni ya kimataifa isiyokuwa na makato ambayo imesaidia kupunguza kiwango cha umasikini’ amesema Bi Rose na kuongeza kuwa hiyo ni muhimu kwa nchi zenye idadi ndogo ya watu.

Kadhalika ameeleza matumaini yake kuwa ziara hiyo itadhihirisha matunda ya kutathimini utekelezaji wa vyombo vya kimataifa kuhusu masuala ya haki za wazee.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter