Kampuni ya Skylon Global ya Kenya kidedea tuzo ya 2017 ya SheTrades

28 Februari 2017

Kampuni ya Skylon Global kutoka Kenya, imeibuka kidedea na kunyakua tuzo ya SheTrades ya changamoto ya uwekezaji kwa mwaka 2017.

Tangazo la ushindi huo lilitolewa mwishoni mwa wiki wakati wa hafla maalumu ya maononyesho ya ufungaji wa kongamano la wanawake wajasiriamali mjini Instanbul Uturuki, ililoandaliwa na kituo cha kimataifa cha biashara ITC. Mkurugenzi wa Skylon Global Hellen Odegi hakuficha furaha yake ya ubunifu uliompa tuzo

(HELLEN CUT)

“Ninajihisi vizuri sana, nimetengeneza app ya simu za rununu ambayo itaunganisha sekta ya afya na wagonjwa, ili kuwe na ujumuishwaji zaidi katika soko na kusaidia kuwafikia wagonjwa ambao hawafikiwi na pia kutoa ajira kwa wanawake. Tayari nina appu kwenye wavuti na hatua inayofuata ni kuanza kupata wateja na kuanzisha app ya simu za andoid”

Zimba Group, kampuni inayohusiana na masuala ya teknolojia ITC kutoka Ugnda ilishika nafasi ya pili kwa sababu ya wazo lake la utengenezaji wa appu itakayo toa fursa ya soko nafuu na kusaidia kujenga uwezo miongoni mwa wanawake wajasiriamali. Sherifa Tumisiine ni mkurugenzi wake

(CUT SHERIFA)

“Nnajivunia kushika nafasi ya pili, hivyo mafunzo na ujuzi ninaoupata kutoka ICT utasaidia kupanua zaidi wigo wa biashara yangu na wajasiriamali wengine watafute fursa kama hizi wajisajili zaidi tukikuwa 36  tu tuliojaza na wanawake zaidi wajitokeze kujaza vitu kama hivi”

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud