Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MINUSCA yazuia mapambano kati ya vikundi vya waasi Bambari

MINUSCA yazuia mapambano kati ya vikundi vya waasi Bambari

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA umeripoti kuwa, Jumapili baadhi ya wanachama 40 wenye silaha wa kikundi cha waasi cha FPRC walikuwa kilometa chache kaskazini ya mji wa Bambari. Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa Katibu mkuu, vikozi vya MINUSCAilibidi vizuie mgogoro kati ya kikundi hicho na kile cha UPC katika mapambano ya angani ambapo watu saba walijeruhiwa, watatu kukamatwa na mmoja kufariki dunia.

Taarifa hiyo imesema waliokamatwa watahojiwa na mamlaka ya mahakama. MINUSCA kwa mara nyingine imetoa wito wa kukomeshwa kwa haraka uadui na kurudia uamuzi wake wa kutumia njia zote zilizoidhinishwa na Baraza la Usalama za kuzuia mapigano Bambari na imepinga shinikizo la FPRC kuzuia wakimbizi wa ndani katika eneo la Ippy, mashariki ya Bambari kutoka kwenye eneo hilo.