Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi na wahamiaji wanakabiliwa na hatari kubwa wakijaruibu kuingia Ulaya:UNHCR

Wakimbizi na wahamiaji wanakabiliwa na hatari kubwa wakijaruibu kuingia Ulaya:UNHCR

Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR inaainisha athari za ongezeko la vikwazo mipakani vilivyoanzishwa mwaka 2016 , kwa wakimbizi na wahamiaji wanaojaribu kuingia Ulaya.

Ripoti hiyo inaonyesha kwamba watu wanaendelea kuhama lakini sasa wanatumia njia mbalimbali na za hatari zaidi, huku mara nyingi wakiwategemea wasafirishaji haramu kwa sababu kwa sababu ya kukosa njia halali za kisheria za kuingiza Ulaya.

Shirika hilo linasema baada ya kufungwa kwa njia ya kupitia Magharibi mwa Balkan na baada ya tamko la Muungano wa Ulaya na Uturuki 2016 , idadi ya watu wanaoingia Ugiriki kupitia Mashariki mwa Mediterranean kutoka afrika ya Kaskazini kwenda Italia sasa ndio imekuwa njia kuu ya kuingia Ulaya. Jumla ya watu 181,436 waliwasili Italia 2016 kwa njia ya bahari kati ya asilimia 90 ya waliosafiri kwa boti kutoka Libya.

URipoti inasema mraia wa mataifa mawili yalikuwa na idadi kubwa ya wanaowasili Italia ambayo ni Nigeria na Eritrea huku idadi ya watoto wakiwa peke yao imeongezeka sana na kufikia zaidi ya 25,000 mwaka 2016.