Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yasajili wahitaji msaada Unity Sudan Kusini

WFP yasajili wahitaji msaada Unity Sudan Kusini

Maelfu ya wanaokabiliwa na njaa katika jimbo la Unity nchini Sudan Kusini wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya usajili wa kupokea msaada wa chakula, baada ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), na wadau wake kutangaza baa la njaa katika sehemu nyingi za nchi hiyo wiki jana. John Kibego na Taarifa kamili.

(Taarifa ya Kibego)

Wameshuhudiwa wakati ambapo watu zaidi ya laki moja nchini humo wanakabiliwa na njaa iliokithiri huku asilimia arobaini yao wakihitaji msaada wa kibinadamu kwa dahrura.

Watu hao walijitokeaza katika Kaunti ya Leer, moja wapo ya Kaunti nne mlimotangazwa njaa katika Jimbo la Unity, na kutunga foleni ndefu kwenye kutuo caha usajili kilicho karibu nao cha Thonyor Payam, wakiwa wametembea safari ndefu kutoka vijijini kwao kufikia kituo hicho.

Imekuwa ni mara ya kwanza ya WFP na wadau wake kufikia eno hilo ambalo halijafikika kwa kipindi kirefu kufatia kuzorota kwa hali ya usalama.