Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

TFV inarahisisha kazi za ICC- Jaji Silvia

TFV inarahisisha kazi za ICC- Jaji Silvia

Rais wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC Jaji Silvia Fernández de Gurmendi ambaye yuko nchini Uganda kwa ziara ya wiki moja amesema anaunga mkono mfumo wa kusaidia wahanga wa uhalifu akisema unasaidia kufanikisha kazi ya mahakama hiyo.

Amesema hayo wakati akizungumza na wanufaika wa miradi itokanayo na mfuko wa kusaidia waathirika hao, TFV huko Gulu nchini Uganda, miradi ambayo inawapatia usaidizi wa kisaikolojia kutokana na mzozo kaskazini mwa Uganda.

(Sauti ya Juaji Silvia)

“Ninaunga mkono kwa dhati miradi ya TFV na ninaamini kuwa ni muhimu kwa sababu uwezo wake wa kuondoa makovu, kupunguza machungu, kusaidia na kulipa fidia wahanga ni sehemu muhimu ya mfumo wa ICC.”

Katika ziara hiyo Jaji Silvia amefungua mahakama ya mashinani ya ICC na pia amekuwa na mazungumzo na wafanyakazi wa mahakama hiyo na wale wa Umoja wa Mataifa.

Atakutana pia na viongozi wa serikali ya Uganda.