Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zichukuliwe kuwalinda watu wa Rohingya Myanmar :UM

Hatua zichukuliwe kuwalinda watu wa Rohingya Myanmar :UM

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Myanmar ametoa wito wa serikali ya nchi hiyo kuchukua hatua haraka kukomesha madhila kwa jamii ya watu wa Rohingya nchini humo.

Akizungumza mwishoni mwa ziara yake ya siku nne nchini humo alikozuru Dhaka na Cox’s Bazar, mwakilishi huyo Yanghee Lee amesema kiwango cha ghasia na ukatili wakinachokabili familia za jamii hiyo ni kikubwa sana kuliko alivyodhani awali.

Katika ziara hiyo amekutana na watu wa jamii ya Rohingya ambao walikimbilia Bangladesh baada ya tarehe 9 Oktoba mwaka 2016 kituo mpakani cha cha polisi wa Myanmar kushambuliwa na kuzuka machafuko.