Skip to main content

WHO yaongeza msaada Somalia kwa waathirika wa ukame

WHO yaongeza msaada Somalia kwa waathirika wa ukame

Shirika la afya duniani WHO linaongeza shughuli zake za msaada nchini Somalia ili kutoa huduma muhimu ya afya inayohitajika kwa watu milioni 1.5 walioathirika na ukame na ongezeko la mgogoro wa chakula.

Hata hivyo WHO imesema inahitaji haraka dola milioni 10 kama sehemu ya ombi la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya miezi sita ya mwanzo wa mwaka 2017.

Hali ya kibinadamu Somalia inazidi kuzorota na kuna hatari kubwa kwamba nchi hiyo itatumbukia kwenye baa la njaa la tatu katika miaka 25.

Zaidi ya watu milioni 6.2 ikiwa ni nusu ya watu wote wa taifa hilo wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu ikiwemo takriban watu milioni 3 wanaokabiliwa na uhaba wa chakula.