Zaidi ya dola milioni 600 zaahidiwa kulisaidia bonde la ziwa Chad

Zaidi ya dola milioni 600 zaahidiwa kulisaidia bonde la ziwa Chad

Jumuiya ya kimataifa leo imesikia kilio cha mamilioni ya watu wa bonde la ziwa Chad ambao wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na madhila mengine ya vita ukiwemo uasi wa kundi la Boko Haram. Ijumaa ya leo kwenye mkutano wa kimataifa wa usaidizi wa eneo la bonde hilo ahadi za mamilioni zimetolewa kwa ajili ya miaka mitatu ijayo. Akizungumza na wanadishi wa habari mwenyeji wa mkutano waziri wa mambo ya nje wa Norway  Børge Brende  amesema

(SAUTI YA BRENDE)

“Nchi 14 zimekuja na ahadi leo na pia tunatarajia ahadi zaidi, nina furaha na kuguswa kutangaza kwamba leo tkumekuwa na ahadi za dola za kimarekani milioni 672 kwa miaka mitatu ijayo, na ahadi kwa mwaka huu wa 2017 dola za Marekani milioni 457 nadhani hii ni habari njema”

Nigeria moja ya nchi nufaika na msaada wa leo, baada ya tangazo la ahadi hizo kupitia waziri wake wa mambo ya nje Geoffrey Onyeama imeishukuru jumuiya ya kimataifa

(SAUTI ONYEAMA)

“Tunashukuru sana na hatuchukulii chochote kwa mzaha, hili ni janga kubwa linalotokea mbele ya macho yetu na ilikuwa muhimu kwa jumuiya ya kimataifa kutambua ukumbwa wa zahma hii”

Naye mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Stephen O’Brien akiwa kwenye mkutano huo amesisitiza umuhimu wa msaada wa jumuiya ya kimataifa

(SAUTI YA O’BRIEN)

"Kuanzia leo familia zilizoathirika na jamii zinazowahifadhi ambazo mara nyingo nazo zina vitu kidogo au hazina chochote, tusipojikakamua wote watakabiliwa na maisha maisha ya njaa hata baa la nja katika baadhi ya sehemu za Mashariki mwa Nigeria, maradhi , ukatili wa kijinsia, watu kueendelea kutawanywa na watoto watakabiliwa na mustakhbali usio na elimu, utapia mlo na kulazimishwa kuingia kwenye vikundi vyenye silaha na vifo vya mapema”