Onyesho la utambulisho wa jamii ya Bhojpuri nchini Mauritius

24 Februari 2017

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO linaendelea na kazi yake ya kubaini tamaduni za aina yake ulimwenguni ambazo zinapaswa kuhifadhiwa ili ziweze kuendelea kurithiwa kizazi na kizazi. Mojawapo ni nyimbo za kiasili "Geet-Gawai" ambazo jamii ya Bhojpuri huimba katika sherehe za kabla ya harusi na tayari UNESCO imeziingiza katika orodha ya turathi za tamaduni zisizogusika za kibinadamu. Ungana na Selina jerobon katika makala ifuatayo...