Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usawa wa elimu

Usawa wa elimu

Usawa wa elimu! Lengo hili linataka uwepo wa elimu jumuishi, yenye usawa, na kupigia chepuo fursa za muda mrefu za kusoma kwa watu wote bila kujali jinsia, hali ya mwili au tofauti yoyote. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, watoto milioni 59 ambao wana umri wa kujiunga na elimu ya msingi, hawajajiunga. Miongoni mwa watoto hao milioni 59, mmoja kati ya watano aliacha shule huku wawili kati ya hao watano ambao hawajajiunga shuleni wakitajwa kuwa kamwe hawatajiunga.

Barani Afrika takwimu za mwaka 2014 zinasema kuwa kati ya silimia 40 na 90 ya watoto walishindwa  kufikia kiwango kidogo cha ustadi wa kusoma . Katika nchi 10 za bara hilo na tisa kati ya hizo, takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 40 na 90 walishindwa kufikia kiwango cha chini cha ustadi katika hesabu.