Skip to main content

Viazi vitamu vinavyohimili ukame kuanza kupandwa Somalia: IOM

Viazi vitamu vinavyohimili ukame kuanza kupandwa Somalia: IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na shirika la maendeleo ya elimu na kilimo vijijini READO, wanazindua kilimo cha viazi vitamu vinavyohimili ukame ambavyo vitasaidia kupunguza athari za ukame nchini Somalia. Grace Kaneiya na taarifa kamili

(TAARIFA YA GRACE)

Ukame uliozuka hivi karibuni nchini humo umewaacha watu zaidi ya milioni 6.2 wakihitaji msaada wa kibinadamu. Mradi huo wa viazi unawalenga zaidi wakimbizi wa ndani na jamii zinazowahifadhi mjini Baidoa ambao watapatiwa mafunzo ya jinsi gani ya kulima viazi hivyo kabila ya kupewa miche na vifaa ambavyo watavitumia katika mashamba yao.

Aina hiyo ya viazi vitamu mara nyingi hujulikana kama orange flesh sweet potato (OFSP),na vinafaa kupandwa kwenye maeneo yaliyo na kiwango kidogo cha mvua.