Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Njaa ya Nigeria sasa yatapakaa bonde la ziwa Chad-FAO

Njaa ya Nigeria sasa yatapakaa bonde la ziwa Chad-FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO limeonya kwamba hali ya uhakika wa chakula nchini Nigeria na bonde la ziwa Chad inazidi kuzorota.Taarifa kamili na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Sasa shirika hilo linatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua haraka kulinda maisha ya mamilioni ya familia ambazo zinategemea kilimo, ufugaji na uvuvi kwa ajili ya chakula na kukidhi mahitaji ya maisha.

Mtafaruku huo wa chakula sasa unahusisha nchi nne, Cameroon, Chad, Niger na Nigeria. Daniele donate ni naibu mkurugenzi wa FAO kitengo cha dharura anafafanua sababu ya kuzorota zaidi kwa hali

(SAUTI DANIELE)

“Machafuko yaliyosababishwa na uasi wa Boko Haram yamesababisha wimbi kubwa na watu kuondoka nah ii imefanya kupungua kwa uzalishaji katika maeneo ya kilimo, na pia kupanda kwa kasi kwa bei ya chakula, lakini pia kutokuwepo usalama kumepunguza uwezekano wa Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu kuingilia kati na kusaidiwa watu hawa”