Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Orlando Bloom akutana na waathirika wa Boko Haram Niger:UNICEF

Orlando Bloom akutana na waathirika wa Boko Haram Niger:UNICEF

Balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF UNICEF Orlando Bloom wiki hii amekuwa safarini mjini Diffa, Kusini Mashariki mwa Niger, ili kutanabaisha mgogoro wa kibinadamu unaonendelea katika bonde la ziwa Chad ambako ghasia za Boko Haram zimesababisha maelfu ya watu kuzikimbia nyumba zao na kuishia makambini.

Maelfu ya watoto pia wamelazimika kufungasha virago, kuacha shule na kujikuta katika hatari kubwa ya utapia mlo. Akiwa njiani kuelekea kambini mjini Diffa Bloom anaeleza alichoshuhudia.

(BLOOM CUT)

“Wakati tunasafiri katika barabara hii unaona mamia ya jamii ambazo ni wakimbizi na wahamiaji wanaotoroka Boko Haram, ni maeneo ya wazi na kukame, huwezi kujua wanafanyaje kwa ajili ya chakula na maji. Hakuna vitu vingi hapa hivyo inaonekana maisha ni magumu sana hapa “

Bloom alipowasili kwenye kambi ya wakimbizi na wahamiaji alikutana na watu mbalimbali akiwemo mtoto Amada Goni mwenye umri wa miaka 14 anayeishi na wazazi wake kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Garin Wazam. Amada amemweleza bloom mgogoro ulipoanza marafiki zake wengi walijiunga na Boko Haram, na yeye amesalia na majinamizi kila alalapo isipokuwa akienda kucheza tu

(AMADA CUT)

“Nikienda kucheza najihisi vizuri , ninajihisi ahueni , inanisaidia kupunguza majinamizi”

Jimbo la Diffa linahifadhi wakimbizi wa ndani 240,000 wakiwemo watoto 160,000.