Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Heshimuni haki za kimataifa CAR: UM

Heshimuni haki za kimataifa CAR: UM

Umoja wa Mataifa umezitaka pande kinzani katika majimbo ya Ouaka na Haute nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kuheshimu sheria za kimataifa kwa kulinda raia na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia wahitaji.

Kwa mujibu wa mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini humo Aboubacry Tall, tangu mwanzo wa mwaka 2017, kumekuwa na mapigano makali kati ya vikundi vyenye silaha katika majimbo hayo ambapo raia wamelazimika kuhama makazi yao.

Akitoa mfano amesema Bambar ambao ni mji mkuu wa jimbo la Ouakani, wenye idadi ya watu 160,000, kwa sasa una watu 45,000 ambao wamefurushwa makwao huku idadi ya wakimbizi wa ndani ikizidi kuripotiwa .

Bwana Aboubacry amesisitiza kwamba machafuko hayo yamesababisha uvunjifu mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu na haki za binadamu, huku vitendo vya unyanyapaa na kunyimwa haki ya kuhama kutoka eneo moja hadi nyingine vikishuhudiwa.