Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama barabarani ni haki ya binadamu-Zeid

Usalama barabarani ni haki ya binadamu-Zeid

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa, Zeid Ra'ad Al-Hussein aliyehudhuria tamasha la filamu kwa ajili ya usalama barabarani amesema aliwahi kupata ajali barabarani, "na kama isingekuwa kwa ajili madaktari waliookoa maisha yake, leo hii asingekuwa hapa.

Zeid amesema hayo wakati wa hafla ya kutangaza washindi wa filamu kuhusu usalama barabarani, hasa kuendesha gari ukiwa umelewa na kuendesha gari ilhali ukiwa umetingwa na mambo mengine liliyofanyika jijini, Geneva, Uswisi.

Filamu hizo zenye lengo la kuchagiza na kuhamasisha sheria kali dhidi ya wahalifu pamoja na kuelimisha umma kuhusu hatari hizo, zinaonyesha jinsi matumizi ya simu za mkokoni zyalivyoongeza athari barabarani ikilinganishwa na na hatari zingine.

Akihutubia washiriki wa ngazi ya juu waliohudhuria hafla hiyo Zeid amesema..

(Sauti ya Zeid)

"Nimegundua kwa umakini kuwa usalama barabarani ni suala la haki za binadamu. Wanadamu wote wanahaki ya kutembea kwa uhuru bila ya kupatwa na janga ".