Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa afya umesambaratika Yemen, mamilioni hatarini kwa utapia mlo na magonjwa:

Mfumo wa afya umesambaratika Yemen, mamilioni hatarini kwa utapia mlo na magonjwa:

Nchini Yemen kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO, wafanyakzi wauguzi mahospitalini hawajalipwa mishahara yao kwa mwezi wa tano sasa . Kuna upungufu mkubwa wa dawa , huku mafuta yakihitajika kwa ajili ya kuhakikisha umeme unafanya kazi hospitali.

Dr Khaled Suhail, mkurugenzi wa hospitali ya Al-Tharwa ambayo ni hospitali ya mji wa tatu kwa ukumbwa nchini Yemen wa Al-Hudaydah anasema , hospitali hiyo ikiwa na wahudumu wa afya zaidi ya 1200 na vitanda 320 ndio hospitali kuu inayofanya kazi na kutoa huduma mjini Al-Hudaydah na majimbo mengine ya jirani.

Kila siku watu takriban 1500 wanafuta huduma ya afya hospitalini hapo. Machafuko katika eneo hilo yameleta athari nyingi ikiwemo kupanda kwa gharama za chakula, dawa, na kupungua kwa shughuli za kiuchumi, na matokeo yake wagonjwa wengi wanashindwa kulipia gharama ndogo za matibabu hospitalini hapo.