Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bunge la Malawi lapitisha mabadiliko ya katiba kukomesha ndoa za utotoni

Bunge la Malawi lapitisha mabadiliko ya katiba kukomesha ndoa za utotoni

Kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya wanawake UN Women kimesema Malawi moja ya nchi zenye kiwango kikubwa cha ndoa za utotoni duniani imechukua maamuzi ya kihistoria bungeni katika kuelekea kwenye usawa wa kijinsia kwa kupiga marufuku ndoa za utotoni. Taarifa kamili na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora)

Kwa mujibu wa kitengo hicho tarehe 14 Februari kwa kauali moja bunge la Malawi lilipitisha marekebisho ya katiba ambayo yanaongeza umri wa kufunga ndoa kutoka miaka 15 hadi miaka 18 kwa wasinana na wavulana.

UN Women imekuwa na mchango mkubwa katika kuchagiza ukomeshaji wa ndoa hizo za utotoni ambazo vitendo vya kibaguzi.

Imekuwa ikiisaidia Malawi wakati wa mchakato mzima wa mabadiliko hayo ya katiba huku ikiyachagiza mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kushirikiana na wizara ya haki na katiba na ile ya wanawake na sheria nchini humo ili kuhakikisha kila upande umeshirikishwa.