Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kambi yafunguliwa Uganda kuhifadhi wakimbizi wa Sudan Kusini

Kambi yafunguliwa Uganda kuhifadhi wakimbizi wa Sudan Kusini

Nchini Uganda, Kambi mipya ya wakimbizi imefunguliwa kaskazini-magharibi mwa nchi, ili kuhifadhi baadhi ya maelfu ya wakimbizi wanaozidi kukimbia makwao nchini Sudan Kusini. John Kibeog an taarifa kamili.

(Taarifa ya Kibego)

Shirika la Umoja Wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na Wadau wake wamefungua kambi ya Imvepi wilayani Arua ikiwa ni miezi miwili baada ya kufunguliwa kwa kambi ya Palorinya wilayani Moyo, ambayo kwa sasa inahifadhi wakimbizi zaidi ya 135,000 wa Sudan Kusini.

UNHCR imesema tayari wakimbizi zaidi ya 2,000 wamepatiwa hifadhi kwenye kambi ya Imvepi inayotazamiwa kuhifadhi zaidi ya 110,000.

Uganda ni nyumbani kwa karibu nusu ya wakimbizi zaidi ya milioni moja nukta tano wa Sudan Kusini waliokimbilia nchi jirani kufuatia kuibuka kwa mzozo wa kisiasa.

UNHCR, imeipongeza Uganda kwa kuendelea kuwapokea, ikisema ni mfano wa kuigwa.