Skip to main content

Wanawake wa Syria nao wapaza sauti vita iishe

Wanawake wa Syria nao wapaza sauti vita iishe

Awamu ya nne ya mazungumzo kuhusu Syria ikiwa imeanza leo huko Geneva, Uswisi kati ya upande wa serikali na wapinzani, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo huo Staffan de Mistura amekutana na wanawake ambao wanakesha usiku kucha kutaka suluhu ipatikane ikwemo hatma ya walioswekwa rumande na waliotoweshwa.

De Mistura amesema kundi hilo linajumuisha akina mama, wake na mabinti na wanawakilisha vilio vya wanaume, wanawake na hata wakati mwingine watoto ambao wanakamatwa na serikali au upinzani katika mzozo huo wa Syria.

(Sauti ya de Mistura)

"Wameniletea ujumbe mimi na watu wengine ya kwamba wakati tunaendelea na mazungumzo kuhusu mustakhbali wa Syria, hatupaswi kusahau wale ambao pengine bado wanashikiliwa au wametekwa kwa sababu kuna maelfu na maelfu ya akina mama, wake na mabinti ambao wanatumai kuwa hoja hii angalau itafapata suluhu kwenye mashauriano.”