Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Heri nusu shari kuliko shari kamili-O’Brien/ Clark

Heri nusu shari kuliko shari kamili-O’Brien/ Clark

Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura bwana Stephen O’Brien amesema katika kukabiliana na tatizo la njaa linalozigubika nchi nne za Sudan kusini , Somalia, Yemen na Nigeria ni bora kuchukua hatua sasa ikiwa nusu shari kuliko shari kamili.

(O’BRIEN CUT)

image
Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura bwana Stephen O’Brien.(Picha:UM/Rick Barjonas)
“Baa hili la njaa linaweza kuepukika kama tutachukua hatua sasa somo kutokana na baa la njaa la 2011 nchini Somalia ni kwamba wakati tulipotangaza baa la njaa kama dunia nusu ya watu waliokuwa walikuwa tayari wameshakufahii ndio sababu tunatoa tahadhari sasa ili tuweze kufanya mabadiliko na kuepuka zahma”

Wakizungumza na waandishi wa habari mjini New York kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hii leo naye mkuu wa shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Bi Helen Clark akaongeza.

(SAUTI YA HELEN CLARK)

image
Mkuu wa shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Bi Helen Clark.(Picha:UM/Rick Barjonas)
"Lengo la msingi hapa ni kuokoa maisha katika mazingira yaliyo magumu kabisa na sehemu ya ya kuokoa maisha hayo ni kujenga uwezo wa kuhimi katika siku za usoni, mambo mengi yanafanyika na yale tunayofanya yamekuwa yakipewa kipaumbele na kuongezewa kasi kama fursa ya huduma za msingi za kijamii , kufufua upya maisha ya watu na kuwezesha uwezo wa serikali husika ili wafikishe huduma wanazopaswa kufikisha.”