Skip to main content

Baa la njaa sio hadithi tena tunalishuhudia-Guterres

Baa la njaa sio hadithi tena tunalishuhudia-Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema baa la njaa sasa ni hali halisi ambayo inashuhudiwa katika sehemu kubwa ya Sudan Kusini.

Akizungumza katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari ukimjumuisha mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP Helen Clark, mratibu wa masuala ya binadamu wa Umoja wa Mataifa Stephen O’Br ien na wadau wengine wakiwemo WFP, FAO na UNICEF amesema nia yao leo ni kuutanabaisha ulimwengu hali halisi kwamba

(SAUTI YA GUTERRES )

“Leo hii watu zaidi ya milioni 20 Sudan Kusini , Somalia, yemen , na Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wanakabiliwa na njaa na hawana uhakika wa chakula.Baa la njaa tayari ni hali halisi Sudan kusini”

Guterres ameonya kwamba hali ni mbaya na dunia isipoziba ufa basi italazimika kujenga ukuta

(SAUTI YA GUTERRES )

“Endapo hatua hazitochukuliwa pochukuliwa sasa basi muda si mrefu hali hii itayakumba pia maeneo mengine nan chi zingine, tunakabiliwa na janga na ni lazima tuliepuke kabla halijawa zahma kubwa , kwani linaweza kuzuilika endapo jumuiya ya kimataifa itachukua hatua madhubuti.”

Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa kimataifa na mashirika ikiwemo Bank ya dunia watafanya kila liwezekanalo kunusuru maisha ya watu ikiwemo kuundwa kwa akamati itakayokuwa daraja baina ya Umoja wa Mataifa na mashirika mengine lakini wanakabiliwa na changamoto kubwa.

(SAUTI YA GUTERRES)

"Moja ya vikwazo vikubwa tunavyokabiliana navyo sasa ni fedhaza ufadhili. Operesheni za kibinadamu katika matifa haya manne zinahitaji zaidi ya dola bilioni 5.6mwaka huu na tunahitaji angalau dola bilioni 4.4 ifikapo mwisho wa Machi ili kuepuka zahma”

Amesema upungufu huo umeyafanya baadhi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo WFP kupunguza mgao wa chakula na hali itakuwa mbaya zaidi miezi ijayo.