Hali tete DRC, MONUSCO yadhibiti

Hali tete DRC, MONUSCO yadhibiti

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokarasia ya Kongo DRC umesema hali ya kiusalama jimboni Kinshasa na maeneo mengine ya kati na mashariki mwa taifa hilo imekuwa tete lakini inadhibitowa.

Akizungumza leo na waandishi wa wa habari msemaji wa kijeshi wa MONUSCO Kanali Serge Haag amesema jeshi lake limedhibiti hali ya uvunjifu wa amani licha ya hali tete hiyo itokanayo na harakati za vikundi vya wanamgambo katika maeneo hayo.

Amesema taarifa zinaonyesha kwamba kumekuwa na utekaji nyara, uporaji wa mali katika baadhi ya maeneo kutokana na harakati za vikundi hivyo kutaka kuyadhibiti baadhi ya maeneo.

Kanali Haag amewahakikishia wananchi kuwa MONUSCO inatekeleza wajibu wa ke wa msingi wa ulinzi wa raia kwa kuhakikisha hali ya amani nchini DRC.